Kuchunguza wa Siasa na Itikadi Katika Tamthiliya ya Nyota ya Tom Mboya

Kitto, John Isaack Batholomayo (2019) Kuchunguza wa Siasa na Itikadi Katika Tamthiliya ya Nyota ya Tom Mboya. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of Kitto-TASINIFU-14-11-2019.pdf] PDF
Download (718kB)

Abstract

Mada ya utafiti huu ilikuwa ni kuchunguza masuala ya siasa na itikadi katika tamthiliya ya Nyota ya Tom Mboya. Lengo kuu la utafiti huu limefikiwa baada ya malengo mahususi matatu kukamilika. Malengo hayo ni Kubainisha siasa zinazojitokeza katika tamthiliya ya Nyota ya Tom Mboya, kubainisha itikadi zinazojitokeza katika tamthiliya ya Nyota ya Tom Mboya na kufafanua uhusiano uliyopo kati ya siasa na itikadi zilizojitokeza katika tamthiliya ya Nyota ya Tom Mboya. Ili kukamilisha malengo haya mahususi, Data za utafiti huu zilikusanywa kwenye kazi teule kwa kutumia mbinu za usomaji na upitiaji nyaraka kwa kina na umakini mkubwa. Aidha data zilichambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na nadharia ya U-marx. Utafiti umebaini kuwa,masuala ya kisiasa nayojitokeza katika tamthiliya ya Nyota ya Tom Mboya ni siasa na harakati za ujenzi wa jamii mpya, uongozi bora na imani kwa wananchi, ukombozi wa nchi za Afrika, elimu na maendeleo, siasa za ukabila, hofu na tamaa ya madaraka, kujitoa muhanga, nafasi ya mwanamke katika siasa, uhusiano wa nchi za Afrika na zile za Magharibi, vibaraka wa kisiasa na umwagaji wa damu. Pia utafiti umebaini kuwepo kwa itikadi katika tamthiliya ya Nyota ya Tom Mboya kama ifuatavyo: itikadi ya ushirika, ujamaa, mapinduzi, ubepari, kikomunisti, dini, utamaduni, mapenzi na ubaguzi wa kijinsia. Yote haya yatatoa mchango mkubwa katika kuimarisha uongozi wa nchi huru za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla kwa kuzingatia katiba za nchi zao.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 800 Literature > 800 Literature, rhetoric & criticism
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 09 Dec 2020 13:21
Last Modified: 09 Dec 2020 13:21
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2606

Actions (login required)

View Item View Item