Kuchunguza Mtindo katika riwaya za Kichwamaji na Kuli: Utafiti linganishi

Haji, Maulid Khatib (2019) Kuchunguza Mtindo katika riwaya za Kichwamaji na Kuli: Utafiti linganishi. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of MAULID SHIRAZ HASSAN.pdf] PDF
Download (1MB)

Abstract

Utafiti huu unahusu kuchunguza mtindo katika riwaya za Kichwamaji (Euphrase Kezilahabi) na Kuli mtunzi (Shafi Adam Shafi). Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni nadharia ya Elimu Mitindo na dhana ya Fasihi Linganishi. Utafiti huu ni utafiti wa maktabani. Data za utafiti huu zimechambuliwa kwa njia ya maelezo ingawa ndani yake kutakuwa na majedwali ambayo yametumika kwa ajili ya kurahisisha kusomeka kwa data kirahisi. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kwamba waandishi wote wawili ni magwiji juu ya utumiaji wa mtindo, wote wametumia tashhisi, tashbiha, mtindo wa majibizano na matumizi ya barua, ingawa kuna utofauti uliosababishwa na mazingira ya waandishi hao au kijiografia, hali hii ndio msingi mkubwa wa kutofautiana kwao. Mwandishi wa riwaya ya Kichwamaji ametumia lugha ambayo alishindwa kupunguza ukali wa maneno na kutumia maneno ambayo ni vigumu kuyatumia au kuyasikia katika kadamu nnasi. Kichwa maji ni riwaya ambayo inazungumzia zaidi juu wa uhasama kati ya Manase (Mkuu wa Wilaya) na Kazimoto (Mwanafunzi wa Chuo Kikuu). Uhasama huo uliaza pale Manase alipompa ujauzito Rukia (mwanafunzi wa shule) mdogo wake Kazimoto. Nae Kazimoto analipiza kisasi kwa Sabina mdogo wake Manase, hatimae kisasi hicho kilibadilika na kuwa furaha. Kuli ni riwaya inayozungumzia juu ya mgomo uliotokea Bandarini Makuli hawakuwa na haki ya kusikilizwa, Makuli walidhalilishwa na walinyonywa, wakipatacho kilikuwa ni kijungu jiko tu. Hali iliyosababisha Makuli kugoma.Katika usawiri wa wahusika mwandishi wa riwaya ya Kichwamaji amewachora wanawake kama ni chombo cha starehe hawana walijualo isipokuwa ni kuwastarehesha wanaume tu, lakini kwa upande wa mwandishi wa riwaya ya Kuli amewachora wanawake kuwa ni wasaidizi wa wanaume kwani wao, ndio waliofanikisha mgomo kutokea baada ya kuwapasha habari Makuli wote baada ya kutumwa kufanya hivyo.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 800 Literature > 800 Literature, rhetoric & criticism
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 09 Dec 2020 13:18
Last Modified: 09 Dec 2020 13:18
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2605

Actions (login required)

View Item View Item