Kuchunguza Dhamira ya Mapenzi katika Riwaya ya Kamwe si Mbali Tena”

Ali, Aisha Mohamed (2019) Kuchunguza Dhamira ya Mapenzi katika Riwaya ya Kamwe si Mbali Tena”. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASINIFU YA AISHA MOHAMED ALI.pdf] PDF
Download (894kB)

Abstract

Utafiti huu ulidhamiria kuchunguza dhamira ya mapenzi katika Riwaya ya Kamwe si Mbali Tena ya Said Ahmed Mohamed. Ili kutimiza lengo kuu hili kulikuwa na malengo mahususi mawili ambayo ni: Kubainisha dhamira ya mapenzi namna ilivyojitokeza katika riwaya ya Kamwe si Mbali Tena na Kuchambua mbinu za kisanaa zilizotumika kuwasilisha dhamira ya mapenzi katika riwaya ya Kamwe si Mbali Tena. Ili kupata data toshelevu zenye kukidhi haja ya matumizi, data za utafiti huu zilikusanywa maktabani kwa kutumia mbinu ya usomaji makini matini na upitiaji wa nyaraka. Data hizo zilichambuliwa kwa njia ya maelezo kulingana na malengo mahsusi yaliyotajwa kwa kuongozwa na nadharia teule ya Mwitiko wa Msomaji kwa lengo la kwanza na nadharia ya Simiotiki kwa lengo la pili. Hatimae matokeo ya utafiti huu yalionesha kuwa dhamira ya mapenzi katika riwaya teule ya Kamwe si Mbali Tena imeweza kujitokeza katika namna tofauti ikiwemo: Mapenzi ya nchi, mapenzi ya familia, mapenzi ya ndoa, mapenzi ya udugu, mapenzi ya urafiki, mapenzi ya dini/imani, mapenzi ya mazingira, mapenzi ya elimu, mapenzi ya mali/pesa na mapenzi ya kazi. Pamoja na hayo pia utafiti umebaini mbinu za kisanaa ambazo zilitumika katika kuwasilisha dhamira hiyo ya mapenzi nazo ni: mbinu ya matumizi ya wahusika, mbinu ya matumizi ya lugha na mbinu ya matumizi ya mandhari. Na mwisho mtafiti amehitimisha kazi yake kwa kutoa mapendekezo faafu kwa walimu, wanafunzi, watafiti wajao na wanajamii kwa ujumla.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 800 Literature > 800 Literature, rhetoric & criticism
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 08 Mar 2021 06:20
Last Modified: 08 Mar 2021 06:20
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2603

Actions (login required)

View Item View Item