Kuchunguza Matumizi ya Tafsida Katika Lahaja ya Kipemba: Uchunguzi wa Mazungumzo

Yussuf, Maua Ame (2017) Kuchunguza Matumizi ya Tafsida Katika Lahaja ya Kipemba: Uchunguzi wa Mazungumzo. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU - MAUA AME YUSSUF.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (1MB) | Preview

Abstract

Utafiti huu ulihusu Kuchunguza Matumizi ya Tafsida Katika Lahaja ya Kipemba. Mtafiti alichagua mada hii ili kuchunguza na kuchambua utajiri mkubwa wa tafsida za lahaja ya kipemba zinavyotumika kwa Wapemba wenyewe. Utafiti huu una lengo kuu moja na malengo mahsusi matatu. Aidha mtafiti alitumia nadharia moja tu nayo ni nadharia ya Simiotiki.Pamoja mtafiti alitumia njia nne za kukusanyia data nazo ni usaili, Uchunguzi makini, Hojaji na mbinu ya maktabani. Data za utafiti huu zilichambuliwa kwa njia ya maelezo, Uchambuzi wa dada ulifanyika kulingana na madhumuni mahususi yaliyotajwa ndani ya utafiti huu. Utafiti umegundua kuwa zipo tafsida za lahaja ya kipembaambazo hutumiwakwa lengo la kuleta heshima katika mazungumzo ya wapemba, lakini pia kulinda na kuendeleza utamaduni wa Wapemba kwa kuzitumia vyema tafsida hizo. Mtafiti amegundua matumizi tofauti ya tafsida ambazo zinatumika na kuleta heshima katika mazungumzo, tafsida hizo ni kama vile kubaua, kujisaidi, utupu/ushi, msalani, kujamiiana (Kuingiliana), mja mzito na mengineyo. Mwisho matafiti amehitimisha kazi yake kwa kutoa mapendekezo kwa wasomi, walimu na wanajamii kwa ujumla kwa kuzilinda na kuziendeleza tafsida, pia kuandaa tafiti nyingine zinazohusu tafsida kupitia lahaja na lughanyingine za makabila.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 470 Italic languages; Latin
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 30 Sep 2018 08:13
Last Modified: 30 Sep 2018 08:13
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2002

Actions (login required)

View Item View Item