Kissassi, Remedius Edington
(2015)
Uubiku Kwa Maendeleo Ya Haraka na Endelevu Zanzibar :Zanzibar.
Medupress, Zanzibar.
Abstract
DIBAJI
Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu nami kupata fursa ya kukisoma kitabu hiki ambacho kimeandikwa na kaka yetu Ndugu Remidius Kissassi.Ukikiangalia utaona ni kidogo kutokana na hali ya uandishi lakini yaliyomo ndani ndio yanathibitisha ukubwa wake kutokana na mambo aliyoyaandika. Masuala ya mahusiano na hali ya kibiashara na ujasiriamali na nadharia nzimayaUbia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Kuondoa Umasikini, kwa kifupi
(UUBIKU)–PPP-PP; ameyaelezea na kuyafafanua vizuri sana.
Kwa mara ya kwanza NduguKissassi aliponiambia anataka kuandika kitabu nikadhani ananifanyia mzaha au dhihaka ingawa nilijua ni mkereketwa mkubwa wa PPP-PP. Pamoja na ukweli kwamba amekuwa karibu sana na wajasiriamali na kusaidia vijana wengi katika mipango yao ya kujinasua na umasikini na kujiletea maendeleo, lakini bado niliona kazi ya kuandika kitabu huhitaji muda na ueledi mkubwa na hasa ujuzi wa fani unayotaka kuiandikia.
Kwa ninavyomfahamu Nd. Kissassi, yeye ni Mhandisi wa shughuli za ujenzi, ingawaanayo shahada yake ya pili ambayo amechukua masuala ya uongozi wa biashara. Pamoja na hayo lakini sikuona la ajabu sana kwani nilijua kuwa yeye mwenyewe ni mfanya biashara na mjasiriamali mzuri na vilevile alishawahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Biashara na Uwekezaji katika Kamati za Bodi ya Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Wakulima (ZNCCIA). Nikajiambia moyoni mwangukuwa,kamaakikusudia kweli basi ataweza kuifanya kazi hii ya uandishi wa mada hii aliyoniambia.
Yalipita masiku bila kuona alichoniahidi na ninapomuliza alikuwa akinijbu “vuta subra Bro”, (akimaanisha mdogo wangu, na hivi ndivyo tunavyoitana kwa maana nami ni kaka yangu) nikimaliza nitakuletea wewe uandike Dibaji; na Kweli muungwana ni vitendo-hatimae kanionyesha kitabu chake. Mimi sina ubavu wa kutia mkono wangu juu ya kazi hii nzuri alojituma kuifanya, lakini naichukulia kama fursa adhimu na adimu kwangu na zawadi aliyonitunikia angalau na mimi niwe sehemu ya kitabu hiki.
Uchumi wa leo umebaini wazi kuwa sekta binafsi ndio muhimili mkuu katika kuusukuma uende mbele lakini unapokuja katika usukumaji huo wa uchumi imeonekana pia sekta binafsi ndio mshirika mkubwa wa sekta za umma.
Zile falsafa za kizamani ambazo zilitegemea sekta ya umma isimamie kila kitu ikiwemo kufanya biasharana utoaji wa huduma, sasa zimepitwa na wakati na hazifai katika zama hizi za Sayansi na Teknolojia. Nchi ambazo bado zinaendelea kung’ang’ania kuwa sekta ya umma iendelee kufanya na kusimamia kila kitu cha uchumi na kijamii hubaki nyuma kimendeleo.
Leo hii tunashuhudia nchi kama China au nchi za mashariki ya Ulaya nk,ambazo mifumo yao ya kiuchumi ilitegemea kuwa shughuli zote zifanywe na sekta ya umma kutokana na sera na siasa za wakati huo lakini sasa tunaona yakuwa nazo zimebadilika.
Ukitaka kujuakwa undani faida na manufaa ya kuwepo kwa ubiana/au mashirikiano mazuri na ya dhati baina ya sekta ya umma na sekta binafsi katika kuondosha umasikini nakusihi ukisome kitabu hiki. Ingawa kinaonekana kidogo ambacho hata ukikusudia kukimaliza kwa muda mfupi utaweza kufanya hivyo lakini hata uelewa na maarifa ya kuifahamu hiyo UUBIKU, pia utaipata kwa muda mfupi; kwahivyo muda mfupi wako utakaotumia katika kitabu hiki utajitosheleza kuchota lulu iliyomo ndani yake.
Napenda Kumshukuru Ndugu yangu Remmy kwa kazi hii nzuri aliyoifanya ambayo faida yake ni kubwana si kwa msomaji tu, bali na hata wale ambao wataguswa kwa namna moja au nyingine na matokeo tarajiwa ya utekelezaji wa mfumo huu.. Ni vizuri basi baada ya msomaji kupata uelewa na kujua manufaa makubwa yakayoweza kupatikana kwa wengi na hasa masikini wa nchi yetu na katika Shehia zote; akafikisha ujumbe huu na yeye akawa Balozi mzuri wa kuona Ubia baina ya sekta za Umma na zile za Binafsi unafanyiwa kazi kwa dhati na kiuhalisia.
Ahsante.
Ali Aboud Mzee
Makamo Wa Rais,
Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wenyeviwanda na Wakulima, Zanzibar.
(ZNCCIA)
Actions (login required)
|
View Item |