Vitenda Will na Ukuaji wa Lugha Nchini Libya na Tanzania

Mohamed, Zeid Abdusalaam (2006) Vitenda Will na Ukuaji wa Lugha Nchini Libya na Tanzania. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of ZUEID_ABDUSALAAM_MOHAMED.pdf]
Preview
PDF
Download (1MB) | Preview

Abstract

Mazungumzo kuhusu vitendawili yamechukua sehemu kubwa ya mambo waliyoyashughulikia wanafasihi wa fasihi ya watu wa zamani. Kwani kila mwandishi wa aina mbalimbali za fasihi alizungumzia vitendawili pamoja na kwamba hawakuandika sana na kwa kina kuhusu vitendawili, ingawa vitendawili huzingatiwa kama moja ya matawi ya fasihi na sanaa asilia yalugha yoyote. Walibya na Watanzania wana vitendawili vya aina mbalimbali katika fasihi simulizi na fasihi pokezi za lugha zao za Kiarabu na Kiswahili, na vitendawili vina mchango mkubwa katika sanaa za lugha mbili hizi. Na kwa sababu hiyo utafiti wetu huu unazungumzia vitendawili na nafasi yake katika kuikuza (kuiendeleza) lugha, na hasa kwa watoto wadogo nchini Libya na Tanzania. Pia utafiti huu unajaribu kuleta ishara sahihi zilizopo katika fasihi, ambazo hutumika katika kufundisha lugha, ikiwa ni ya Kiarabu nchini Libya au ya Kiswahili nchini Tanzania. Utafiti huu unalenga kujua ni pande (sehemu) zipi sahihi ambazo wanazitumia walimu katika kuifundisha lugha kwa watoto kwa ajili ya kupanua uwezo wao wa kufahamu akilini mwao, pamoja na kuendeleza msamiati wa lugha yao. Hivyo suala linalohusu msamiati na maudhui ya vitendawili ni suala la msingi katika kujifunza, kufundisha na kukuza lugha. Utafiti huu umekusanya vitendawili mia moja. Kila moja ya jamii mbili ina vitendawili hamsini, kisha vitendawili vya Libya vimefasiriwa kwa lugha ya Kiswahili ili visomwe kwa urahisi na mzungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Baadaye vimecharnbuliwa kwa lengo la kubainisha mfanano, muundo na maudhui. Utafiti huu unazingatia kuwa ni mwanzo unaofungua njia kwa watafiti wengine ili wafanye tafiti zaidi katika maudhui ya vitendawili, sanaa zake, umuhimu wake na nafasi yake katika kuifundisha lugha.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 200 Religion
Divisions: UNSPECIFIED
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 25 Aug 2011 11:13
Last Modified: 17 Jun 2013 09:35
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/58

Actions (login required)

View Item View Item