Mohamed, Zeid Abdusalaam
(2006)
Vitenda Will na Ukuaji wa Lugha
Nchini Libya na Tanzania.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Mazungumzo kuhusu vitendawili yamechukua sehemu kubwa ya
mambo waliyoyashughulikia wanafasihi wa fasihi ya watu wa zamani. Kwani kila mwandishi wa aina mbalimbali za fasihi alizungumzia vitendawili pamoja na kwamba hawakuandika sana na kwa kina kuhusu vitendawili, ingawa vitendawili huzingatiwa kama moja ya matawi ya fasihi na sanaa asilia yalugha yoyote. Walibya na Watanzania wana vitendawili vya aina mbalimbali katika fasihi simulizi na fasihi pokezi za lugha zao za Kiarabu na Kiswahili, na vitendawili vina mchango mkubwa katika sanaa za lugha mbili hizi. Na
kwa sababu hiyo utafiti wetu huu unazungumzia vitendawili na nafasi yake katika kuikuza (kuiendeleza) lugha, na hasa kwa watoto wadogo nchini Libya na Tanzania. Pia utafiti huu unajaribu kuleta ishara sahihi zilizopo katika fasihi, ambazo hutumika katika kufundisha lugha, ikiwa ni ya Kiarabu nchini Libya au ya Kiswahili nchini Tanzania. Utafiti huu unalenga kujua ni pande (sehemu) zipi sahihi ambazo wanazitumia walimu katika kuifundisha lugha
kwa watoto kwa ajili ya kupanua uwezo wao wa kufahamu akilini mwao, pamoja na kuendeleza msamiati wa lugha yao. Hivyo suala linalohusu msamiati na maudhui ya vitendawili ni suala la msingi katika kujifunza, kufundisha na kukuza lugha. Utafiti huu umekusanya vitendawili mia moja.
Kila moja ya jamii mbili ina vitendawili hamsini, kisha vitendawili vya Libya vimefasiriwa kwa lugha ya Kiswahili ili visomwe kwa urahisi na mzungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Baadaye vimecharnbuliwa kwa lengo la kubainisha mfanano, muundo na maudhui. Utafiti huu unazingatia kuwa ni mwanzo unaofungua njia kwa watafiti wengine ili wafanye tafiti zaidi katika maudhui ya vitendawili, sanaa zake, umuhimu wake na nafasi yake katika kuifundisha lugha.
Actions (login required)
|
View Item |