Omar, Haji Maulid
(2013)
Nafasi ya hadithi Simulizi katika kufunza Maadili mema shule za sekondari, Visiwani Zanzibar.
["eprint_fieldopt_thesis_type_phd" not defined] thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Hadithi Simulizi zimeanza zamani kutumika katika jamii. Hadithi zilikuwa na zinaendelea kutumika katika jamii ya watu wa Visiwa vya Zanzibar katika fani mbalimbali za kimaisha. Wazee majumbani na walimu katika Shule za Sekondari hutumia hadithi simulizi katika kufunza maadili mema. Mtafiti amefanya utafiti katika maeneo mbalimbali na kuona nafasi ya hadithi simulizi katika kufunza maadili mema Shule za Sekondari, Visiwani Zanzibar. Utafiti umefanyika katika maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba. Data zimekusanywa maktabani, katika Shule za Sekondari na Mitaani, kwa wazee, walimu, na wanafunzi. Data kuu alizokusanya mtafiti ni hadithi za ngano, vigano na soga. Sura ya kwanza, inazungumzia usuli wa mada na kugusia nafasi ya hadithi simulizi katika kufunza maadili mema Shule za Sekondari Visiwani Zanzibar, lengo la utafiti, madhumuni mahsusi, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti, eneo na mipaka ya utafiti. Sura ya pili, imebainisha maelezo mafupi ya kazi tangulizi na jinsi zilivyomsadia. Sura ya tatu, utafiti umekusanya nadharia mbalimbali kama vile ndani-nnje, mkabala wa kiislamu, ya fasihi na jamii, ya muundo na ya hisia zinazohusu fasihi simulizi na maadili. Sura ya nne, imefafanua mbinu na njia za utafiti ambazo zimeelezwa ndani ya tasnifu, kuonesha pahala pa utafiti, uteuzi, ukusanyaji wa data, vifaa vya utafiti na uchambuzi wa data. Sura ya tano, imeshughulikia uchambuzi wa data na matokeo ya utafiti. Kwa ujumla mtafiti ametumia nadharia ya Ndani-Nnje, Dhima na kazi ya fasihi, ya Kiisilamu, ya muundo, na ya hisia. Sura ya sita ni uhitimisho na mapendekezo, mtafiti ametoa hitimisho na muhtasari wa mapendekezo ya kazi yake ya utafiti.
Actions (login required)
|
View Item |